Somo limetafsiriwa na Mgune Masatu
(Waebrania 7 & 8, Kutoka 28)
Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2009, Bruce N. Cameron, J.D. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Somo limekaa kimtazamo kwamba mwalimu anatumia ubao au sehemu nyingine yoyote ambayo inaweza kuonekana na wanafunzi. Somo hili pia linaweza kupatikana kutoka http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza pamoja na lugha nyingine kama vile Kifaransa, Kijerumani. Omba kwa ajili ya uongozi wa Roho Mtakatifu unapojifunza.
Utangulizi: Je, huwa unajiuliza kuwa, “Ninajuaje kama Ukristo ni imani sahihi?” Dini ya Kiyahudi ni ya kale. Uislamu ni wa hivi karibuni kuliko dini ya Kiyahudi au Ukristo, lakini unakua kwa kasi. Dini zote “zinahusiana” kwa maana kwamba zote zinatumia kitabu cha aina moja (Agano la Kale la Biblia). Marafiki zangu wa Kiyahudi huniambia kuwa Ukristo umeteka nyara dini yao. Waislamu wanakubali sehemu za Agano la Kale na Agano Jipya. Nadhani ni sahihi kusema kuwa Mtume Mohammed aliamini kuwa alikuwa mtu wa hivi karibuni kabisa (na mkuu) kwenye mlolongo wa manabii wa Agano la Kale. Sehemu kubwa ya jibu limo kwenye somo letu la juma hili kuhusu mfumo wa hekalu. Hebu tuzame kwenye somo letu la Biblia na kuona kile Mungu alichotuandalia!
I. Mkondo/Mwelekeo wa Uthibitisho
A. Soma Waebrania 8:1-5. Je, Musa alijenga hema ya aina gani? (Soma Kutoka 25:8-9 na Kutoka 26:30. Musa alijenga hekalu jangwani. Hii ilifanya muktadha wa ibada ya Kiyahudi. Hekalu la Musa lilielekezwa kwenye hekalu la mbinguni.)
1. Je, lengo la hekalu jangwani lilikuwa lipi? (Ni mahali ambapo Mungu alikaa na watu wake. Lilitoa njia ambayo dhambi za watu zilisamehewa. Angalia Mambo ya Walawi 16.)
2. Pale ambapo Waebrania 8:3 inarejea “kila kuhani mkuu” akitoa “vipawa na dhabihu,” hii inarejea/inanukuu huduma za hekalu za Agano la Kale. Je, marafiki zetu wa Kiyahudi wanapataje msamaha wa dhambi zao hivi leo? (Hilo ndilo tatizo la kimantiki la dini ya Kiyahudi hivi leo. Kutokana na sababu ambazo hazikufunuliwa kwenye Agano la Kale, wameacha mfumo wa utoaji kafara.)
a. Unadhani ni hoja gani waliyo nayo kwa haya mabadiliko? (Hekalu liliharibiwa na Warumi mwaka wa 70 BK. Nilihudhuria Karamu ya chakula cha jioni ya Kiyahudi juma hili, na sehemu ya nukuu ilikuwa ni kwa ajili ya ujenzi mpya wa hekalu.)
b. Je, watu wa Mungu walitoa kafara wanyama wao kwa ajili ya msamaha wa dhambi zao kabla ya utengenezwaji wa hekalu/madhabahu la pale jangwani? (Ndiyo. Soma Mwanzo 8:20. Kimantiki, marafiki zetu wa Kiyahudi bado wanapaswa kuwa wanatoa kafara wanyama wao kwa ajili ya msamaha wa dhambi.)
B. Soma Waebrania 7:23-28. Je, madai yetu ni yapi kuhusu Yesu na mfumo wa hekalu? (Tumeona kwamba mfumo wa hekalu wa Agano la Kale ulikuwa tu ni mwavuli wa hekalu la mbinguni. Utoaji kafara wa Agano la Kale ulikuwa ni mfano (ulitabiri) maisha makamilifu ya Yesu na kafara ya kifo kwa ajili yetu kwa ajili ya msamaha wa dhambi zetu. Yesu sio kafara tu, Yeye ni Kuhani wetu Mkuu akitupatanisha katika hekalu la mbinguni kwa niaba yetu kwa ajili ya msamaha wa dhambi zetu!)
1. Je, sisi tuna hatia kama tulivyoshtakiwa – je, tumeiteka nyara dini ya Kiyahudi? (Dini ya Kiyahudi pasipo kafara ya mnyama ina tatizo la kimantiki. Ukristo una jibu la hilo tatizo – Yesu ndiye utimilifu wa mfumo wa hekalu.)
2. Je, hiyo inauacha Uislamu katika hali gani? Kwa sababu ni dini ya hivi karibuni, je, “inatimiza” dini ya Kiyahudi na Ukristo kwa uzuri zaidi? (Hapana. Uislamu unaukubali mfumo wa hekalu wa Agano la Kale kuwa wa kweli, lakini pia unapungukiwa kafara. Uislamu haukubali kuwa Yesu alikufa na kwamba alifufuka. Hauna hekalu na hauna Mwanakondoo kwa ajili ya ondoleo la dhambi. Hivi leo, Dini ya Kiyahudi na Kiislamu ni dini za “matendo” –kama jinsi zilivyo dini zote za Kimashariki. Wokovu unatokana na matendo ya mwanadamu. Mfumo wa hekalu haumaanishi kitu chochote. )
II. Mavazi na Heshima
A. Je, umewahi kusoma mwisho wa kitabu kwanza? (Mke wangu anafanya hivi mara zote, kamwe sifanyi hivyo.)
1. Je, nini faida ya kusoma mwisho wa kitabu kwanza? (Inaondoa fumbo/siri. Inakusaidia uelewe kitabu unapokuwa unakisoma.)
2. Je, nimefanya hivyo kwako hivi punde? Je, tumesoma mwisho wa kitabu kwanza kwenye somo letu la leo? (Ndiyo, kwa mantiki fulani tulikuwa sahihi kwenye hitimisho la ishara ya mwana kondoo na kuhani mkuu kweye huduma ya hekalu ya Agano la Kale. Hebu tuone kama hii inatusaidia kuelewa vizuri zaidi mavazi ya kuhani mkuu.)
B. Hebu turejee na kusoma Kutoka 28:1-5. Je, lengo la haya mavazi ni lipi? (Kumpatia Haruni “utukufu na uzuri/heshima.”)
1. Soma Kutoka 32:2-4. Je, Haruni alistahili utukufu na heshima? (Hapana.)
C. Soma Luka 15:21-22. Nini lengo la kuvishwa vazi, pete na viatu kwa mwana mdogo? (Kumpatia utukufu na heshima ya uana (kuwa mwana).)
1. Je, mwana mdogo alistahili utukufu na heshima ya kuwa mwana? (Anasema hakustahili.)
D. Soma Mathayo 22:8-12. Kumbuka majuma kadhaa yaliyopita tulijadili hawa wanunuzi wa kwenye maduka kama ya Shoprite wakialikwa kwenye harusi ya mfalme. Je, wageni hawa wanastahili kualikwa? (Kwa hakika hapana kabisa. Tunaambiwa kuwa baadhi yao ni “wabaya.”)
1. Je, nini lengo la kuwapatia vazi la harusi? (kuwapatia utukufu na heshima ambayo ungeitarajia kwa wageni kwenye harusi ya mwana wa mfalme. Walifunika mavazi yao yaliyonunuliwa “Shoprite.”)
E. Je, kuna mantiki inayofanana kati ya vazi la kuhani mkuu, vazi la baba na vazi la harusi? Au, je, ninachanganya matufaa (apples) na machungwa? (Katika sehemu zote tatu, mtu asiyestahili alifanywa kustahili kwa kupatiwa kitu cha kuvaa. Walitakiwa kuboresha hadhi yao ili washerehekee tukio muhimu.)
1. Je, nini kingetokea kama mgeni harusini angekataa vazi la harusi, mwana angekataa vazi alilopewa na baba yake au kuhani mkuu angekataa mavazi yake ya kikuhani? (Tunajua kwa hakika kwamba kuhani mkuu na mgeni harusini wasingeruhusiwa kukaa mbele za Mungu. Mwana mpotevu alitaka kuwa mbele za baba yake, na kwa furaha kabisa alikubali vazi alilopewa na baba yake.)
2. Je, ni somo gani tunalojifunza kutokana na haya mavazi? (Kama tunataka kusherehekea na Mfalme, tunahitajika kuboresha hadhi yetu kwa kuvaa vazi analolitoa Mungu.)
a. Je, hii inatufundisha nini kuhusu dini zote zinazoangalia “matendo?”
III. Utondoti, Utondoti (Taarifa Kamilifu/za Kina, Taarifa Kamilifu/za Kina).
A. Hebu turudi nyuma hadi hadi kwenye Kutoka 28 na kusoma taarifa zaidi kuhusu vazi la kuhani mkuu. Soma kutoka 28:9-12. Kwa kuwa hizi zote ni ishara, je, haya mawe ya ukumbusho yanaashiria nini? (Mara zote Mungu anataka majina ya watu wake mbele zake.)
1. Kwa nini tu usiorodheshe makabila kumi na mawili kwenye ukuta wa hekalu la mbinguni? Ni umuhimu gani unaouona kwenye ishara kuwa kuhani mkuu ana majina yao mabegani mwake? (Hii inaashiria Yesu akibeba dhambi zetu mabegani mwake.)
2. Je, mara zoteunataka jina lako liwe kuu mbele za bosi wako? (Angalia kwenye huo muktadha. Jina linakuja mbele za bosi katika muktadha wa dhambi iliyosamehewa!)
B. Soma Kutoka 28:15-21. Ni somo gani tunalojifunza kutokana na ukweli kwamba majina ya makabila yalichongwa kwenye mawe ya thamani yaliyo katika mfano wa dhahabu? (Sisi ni wa thamani kwa Mungu. Anatuthamini!)
C. Soma Kutoka 28:29-30. Baini majina ya watu wa Mungu sio tu kwamba yanavaliwa kwenye mabega ya kuhani mkuu, yanavaliwa moyoni mwake. Je, ni somo gani tunalojifunza kutokana na hiyo ishara? (Kwa kuwa kuhani mkuu ni ishara ya Mungu, tunajifunza kuwa tuko karibu sana na moyo wa Mungu anapotupatanisha kwa ajili yetu mbinguni.)
1. Mafungu haya yanaanzisha wazo jingine, Urimu na Thumimu. Je, lengo la haya mawe ni lipi? (Soma Hesabu 27:21. Ukweli kwamba kifuko cha kifuani kinaitwa “kifuko cha kifuani cha maamuzi” kilichounganishwa na huu muktadha wa kuyatumia haya mawe kuelewa mapenzi ya Mungu, inatuonyesha kuwa haya mawe mawili yaliwasilisha mapenzi ya Mungu kwa watu wake.)
2. Je, ni ishara gani unazoziona kwenye Urimu na Thumimu? (Chukulia jinsi ambavyo Kuhani wetu Mkuu, Yesu, anavyoangaza/yanavyomulika mapenzi ya Baba kwetu. Kama unataka kujua jibu la Mungu la matatizo magumu maishani, basi mwangalie Yesu.)
IV. Hivi Leo
A. Soma 1 Petro 2:9 na 1 Timotheo 2:5-6. Yesu anatuita kuwa “makuhani wa kifalme,” lakini Paulo anatukumbusha kuwa kuna mpatanishi mmoja pekee, naye ni Yesu. Ukiangalia yote tuliyojifunza kuhusu kuhani mkuu, je, tuhitimishe kuwa jukumu letu ni lipi hivi leo tukiwa kama makuhani? (Dhana ya ukuhani wa uanadamu ilikuwa ni kufunua mpango wa Mungu wa wokovu na kushiriki mapenzi yake pamoja na dunia yote. Baini kuwa 1 Petro 2:9 inatutaka “kuzitangaza fadhili” za Mungu. Huo ndio utume wetu wa kikuhani hivi leo!)
B. Rafiki, je, utakubali na kuufanyia kazi wito wako kuwa kuhani wa Mungu aliye Hai? Je, utashiriki pamoja na dunia kwamba sio matendo yetu yanayotuokoa, bali tu ni kujitegemeza kwenye maisha, kifo na ufufuo wa Mwanakondoo wa Mungu. Je, utaiweka imani yako yote kwenye upatanisho wa Kuhani wetu Mkuu aliyepo kwenye Hekalu la Mbinguni?
V. Juma Lijalo: Joho la Eliya na Elisha.
Monday, April 25, 2011
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Hapa tunajifunza ya kuwa wote tuko sawa mbele ya mungu wwetu hakuna mtu mume wala mtu mke wote ni sawa mbele zake baba wa mbinguni
ReplyDelete