Friday, April 29, 2011

Somo la 6: Joho la Eliya na Elisha

Somo limetafsiriwa na Mgune MAsatu

(1 Wafalme19, 2 Wafalme 2)
Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2009, Bruce N. Cameron, J.D. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Somo limekaa kimtazamo kwamba mwalimu anatumia ubao au sehemu nyingine yoyote ambayo inaweza kuonekana na wanafunzi. Somo hili pia linaweza kupatikana kutoka http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza pamoja na lugha nyingine kama vile Kifaransa, Kijerumani. Omba kwa ajili ya uongozi wa Roho Mtakatifu unapojifunza.

Utangulizi: Je, unakumbuka mchezo wa video wa Donkey Kong? Ingawa ni muda mrefu umepita tangu nilipocheza mchezo wa huo, bado nakumbuka nilivyokuwa nikijaribu kumchezesha Mario hadi kwenye maeneo ya miinuko. Tulikuwa tukipata mafanikio makubwa, na kisha ghafla kupitwa na mifululizo ya mapipa au vitu vingine vya hatari na kujikuta tukiwa nyuma chini kabisa. Je, maisha yako ya kiroho yanafanana na mchezo huo? Mafanikio makubwa yakifuatiwa na anguko kubwa? Mafanikio madogo yakifuatiwa na anguko dogo? Somo letu juma hili ni kumhusu Eliya, mtu aliyeshika kanuni za mchezo wa Donkey Kong. Hebu tuchupe kwenye somo letu la Biblia!

I. Anguko

A. Soma 1 Wafalme 19:1. Je, ni kisa gani alichokielezea Ahabu? (Ukipitia 1 Wafalme 18 utaona kuwa Eliya aliwapa changamoto Ahabu na manabii wa Baali, yaani mpambano wa watu wawili mbele ya mashahidi ya watu wote. Suala lilikuwa ni kuona kuwa nani angeweza kushusha moto kutoka juu pale mlimani: manabii wa uongo 850 na miungu yao au Eliya na Mungu wake? Mungu wa Eliya alishinda, na Eliya aliwaua mamia ya manabii wa uongo. Kwa hakika kilikuwa ni kisa.)

B. Soma 1 Wafalme 19:2. Je, jibu hili ni la busara kwa kiasi gani?

1. Je, ni “miungu” gani kwa hakika aliyokuwa akiinukuu/akiirejea Yezebeli? (Hili ni jibu la kijeuri na la kishupavu. Mungu wa Eliya alishinda kwenye mpambano kati ya Eliya na manabii mbele ya mashahidi na mamia ya manabii wa mungu mshindwa waliuawa. Yawezekana Yezebeli alikuwa amejificha uvunguni mwa kitanda chake kwa kumwogopa Mungu wa kweli.)

C. Soma 1 Wafalme 19:3-5. Kama wewe ungekuwa Mungu, ungewafanyaje Yezebeli na Eliya?

1. Kwa kuwa Yezebeli aliomba kwa uchaji wa miungu, kwa nini tu isimshindie/wasishinde?

2. Kwa nini Eliya anaomba ili kwamba afe?

3. Kama anataka kufa, ingekuwa mantiki angejielekeza kwenye kasri la Yezebeli. Ni hatua gani Mungu achukue kwenye uasi wa kipumbavu (Yezebeli) na mwoga mpumbavu (Eliya)?

4. Je, una kisingizio kwa ajili ya Eliya?(Kuwaua wale manabii wote huenda kulikuwa na athari za kihisia kwake. Msongo kutokana na ule mpanbano mbele za mashahidi ulikuwa na athari kwenye hisia zake. Kwa hakika amechoka, mwenye msongo na mdhoofu.)

5. Je, ni kweli kwamba hastahili joho la kikuhani? Ya kwamba yeye sio bora kuliko watangulizi wake? (Hadi kufikia kwenye uoga, alikuwa mmojawapo wa wapiganaji wakubwa kwa ajili ya Mungu wa majira yote. Yeye ni sura ya mwanadamu mwenye nguvu za Mungu.)

D. Soma 1 Wafalme 19:5-6. Eliya alimwangusha Mungu. Je, Mungu anafanyaje? (Hamtimui Eliya. Anatuma usaidizi. Mungu mkuu wa namna gani tuliye naye!)

E. Soma 1 Wafalme 19:7-8. Kwa nini malaika anamsaidia Eliya kutoroka?

1. Kwa nini asimpige kofi, kumrejesha kwa Yezebeli, na kusema “Pambano liko pale. Acha kukimbia uelekeo usio sahihi.”

F. Soma 1 Wafalme 19:9-10. Kwa nini malaika na Mungu wanaonekana kuwa na majibu tofauti? (Mungu anatupenda na anatujali, lakini pia anatutia hamasa pale tunapokuwa sio waaminifu.)

1. Je, kisingizio cha Eliya ni kipi? Je, anamlaumu Mungu? (Anaamini kuwa yu peke yake. Mungu anahitajika kupata wasaidizi wengine.)

a. Je, hii ni kweli? (Haikuwa kweli pale moto uliposhuka chini pale mlimani.)

b. Je, haya maneno yametoka kinywani mwako ulipofikiri uliwahitaji watu wengine kusaidia kusukuma mbele kazi ya Mungu?

c. Je, ni “sawa” kwa kuhani mkuu wa Mungu kufikiri na kuongea namna hii?

II. Mungu na Anguko
A. Soma 1 Wafalme 19:11-13. Eliya analalamika kwamba yuko peke yake na kwamba amechapwa. Mungu anasema kwamba Eliya anapaswa kutazama gwaride ambapo Mungu atakuwa Grand Marshal. Dhana ya Mungu ni ipi katika hili? (Mungu anadhibiti nguvu za asili.)

1. Je, hilo ni somo jipya kwa ajili ya Eliya? (Hapana. Mjadala uliosababisha mpambano kuhusu moto baina ya pande mbili ulikuwa kwamba watu walikuwa wanamwabudu Baali (mungu mwenye uzao), na Mungu alileta ukame katika nchi.)

a. Kama somo sio geni, kwa nini Mungu analirudia? (Ni mara ngapi unahitaji Mungu arudie masomo yake kwako?)

2. Inamaanisha nini kwamba Mungu hayumo kwenye hizi nguvu kubwa za asili?

B. Baini kuwa Mungu anarudia swali lake la “Unafanya nini hapa” kwa Eliya mwishoni mwa gwaride. Kwa nini?

1. Je, Mungu yu kwenye unong’onezaji wa upole (sauti ndogo ya utulivu)? (Ndiyo. Suala ni kwamba Mungu anadhibiti nguvu za asili, lakini hawadhibiti watumishi wake!)

2. Kwa nini Eliya anafunika uso wake kwa joho lake mbele za sauti ndogo ya utulivu, lakini sio ambapo miamba ilipokuwa inavunjikavunjika na kurushwa? (Alitambua uwezo wa kweli wa Mungu.)

C. Soma 1 Wafalme 19:14. Je, Eliya alipaswa kurudia jibu lake lile lile la awali? (Halionekani kukaribia kuwa jibu zuri baada ya mwonekano wa huu uwezo.)

1. Unadhani Mungu alihitaji jibu gani? (Samahani kwa kukuangusha, sijui nilichokuwa nikikifikiria, nitarajea na kumkabili Yezebeli.”)

D. Soma 1 Wafalme 19:15-18. Hebu jiweke kwenye nafasi ya Mungu. Je, utamwambia nini Eliya katika hatua hii? Je, sasa utamtimua?

1. Je, Mungu alimtimua Eliya? (Anamweka kwenye mpango wa kustaafu. Mungu anamwambia Eliya kuwa atamteua mrithi wake.)

2. Je, utashauri kumwambia Mungu kuwa unataka kuachia ngazi?

E. Soma sehemu ya kwanza ya 1 Wafalme 19:19. Je, hii ni muhimu/ina maana? (Ndiyo. Eliya aweza kuwa anasema mambo yasiyokuwa sahihi, lakini anakwenda pale Mungu alipoelekeza. Anamchagua Mungu na sio kifo/mauti.)

F. Soma 1 Wafalme 19:19-21 na Hesabu 20:23-29. Nini umuhimu wa Eliya kumvika Elisha joho lake? (Ni ishara ya kupasisha mamlaka.)

1. Je, ilikuwa muhimu kwamba Eliya alitupa tu joho lake kwa Elisha, kinyume na kumpatia mavazi yake yote? (Tofauti na Haruni, Mungu hakuwa anambadilisha Eliya mara moja. Badala yake, Elisha alitumika kama msaidizi wa Eliya kwa muda fulani.)

G. Fikiria mfululizo huu kwa dakika moja hivi. Kama wewe ungekuwa Mungu, je, ungembadilisha Eliya kutokana na imani yake iliyoanguka/iliyofifia?

1. Je, ubadilishwaji wa Eliya ulikuwa na vingi vya kujihusisha na msemo wake wa “Nataka uiondoe roho yangu,” au anguko lake la imani?

2. Unalinganishaje hili na Haruni, ambaye hakuonekana kutaka kubadilishwa? (Haruni amekuwa akijihusisha kwenye dhambi nzito mara kadhaa. Eliya alikatishwa tamaa sana – lakini aliamua kuifuata njia ya Mungu. Mungu alimpatia Eliya msaidizi kumsaidia kubeba mzigo wake. Ingekuwa bora zaidi kwa Eliya kuomba kwa ajili ya msaidizi, sio kifo/mauti.)

III. Thawabu

A. Soma 2 Wafalme 2:1-3 na Mwanzo 5:23-24. Unadhani manabii walifikiria kuwa nini kitatokea kwa Eliya?

1. Unadhani Elisha alifikiria kuwa nini kitatokea? (Hakutaka kukiongelea. Hakuna hata mmoja baada ya Henoko alitwaliwa, kwa hiyo nadhani alifikiri kuwa Eliya atakufa siku hiyo.)

2. Ruka na usome 2 Wafalme 2:16-17. Hii inafunua kwamba manabii hawakuwa na wazo kuwa Eliya alikuwa anakwenda kuchukuliwa mbinguni. Lazima watakuwa wamefikiria kuwa alikuwa anakwenda kufa.)

B. Soma 2 Wafalme 2:7-10. Kwa nini hili ni jambo gumu? (Elisha anamwomba Eliya amdhibiti Mungu.)

1. Unafikiria nini kuhusu jibu la Eliya la “hebu tungoje tuone?” (Eliya alimwachia Mungu jambo hilo.)

2. Je, umewahi kumwomba Mungu kitu fulani hivi chepesi – kama vile akusaidie kupata funguo zako – na kujisikia hatia kwa sababu watu wengine walikuwa wanamwomba awaponye saratani?

a. Je, hili suala la “kuyapiga maji na yakagawanyika” linapendekeza nini kuhusu uwezo wa Mungu? (Uwezo wa Mungu upo kwa ajili ya mambo madogo na mambo makubwa. Sio kwamba uwezo wa Mungu unaotumika kukusaidia kupata funguo zako unampokonya/unamnyima mtu mwenye saratani uwezo wa Mungu.)

C. Soma 2 Wafalme 2:11-12. Fikiria pale nyuma ambapo Eliya alikata tamaa na akataka kuondoka na kufa. Nadhani manabii walifikiri hii ndio ilikuwa siku ya kifo chake. Je, hii inasema nini kuhusu upendo wa Mungu wetu? (Anatupatia uzima, sio kifo! Upendo wa ajabu namna gani!)

D. Kumbuka kwamba Mungu alimpa changamoto Eliya kwa kile alichokuwa anakifanya. Je, huyu ni mtu ambaye ungempa thawabu kwa kumchukua moja kwa moja mbinguni? (Mungu anajua kuwa sisi ni wanadamu wadhaifu. Eliya alikuwa mbia mkubwa wa Mungu. Baada ya “anguko” lake, alirejea kwenye njia sahihi na aliendelea kumtumikia Mungu kwa uaminifu. Mungu mkarimu namna gani tuliye nae!)

1. Baini tena 2 Wafalme 2:12. Je, Elisha amefurahi sana kiasi kwamba anaongea mambo yasiyokuwa na maana? Je, anawaona askari? (Kile anachokisema Elisha ni cha muhimu sana. Mtu aliyejazwa na Roho ana nguvu/uwezo zaidi kuliko jeshi la daraja la kwanza.)

E. Soma 2 Wafalme 2:13-15. Elisha anachukua joho na anararua mavazi yake yaliyozeeka. Je, hii inamaanisha nini/ni ishara ya kitu gani? (Manabii walikisema kile inachomaanisha – Roho wa Mungu sasa yupo juu ya Elisha.)

F. Rafiki, je, unajihisi kama unamwangusha Mungu nyakati zingine? Mungu sio tu kwamba anakupenda, bali anakupatia uwezo mkubwa wa kuutafuta/kufikia ufalme wa Mungu – uwezo wa Roho wake Mtakatifu. Je, utaomba hivi leo ili kupewa huo uwezo?

IV. Juma Lijalo: Katika Uvuli wa Mbawa Zake.

0 comments:

Post a Comment