Friday, August 26, 2011
Somo la 10: Ibada: Kutoka Uhamishoni Hadi Urejeshwaji
Somo Limetafsiriwa na Mgune MAsatu
(1 Wafalme 8, Ezekieli 8 & 9, Yeremia 29)
Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2009, Bruce N. Cameron, J.D. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Somo limekaa kimtazamo kwamba mwalimu anatumia ubao au sehemu nyingine yoyote ambayo inaweza kuonekana na wanafunzi. Somo hili pia linaweza kupatikana kutoka http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza pamoja na lugha nyingine kama vile Kifaransa, Kijerumani. Omba kwa ajili ya uongozi wa Roho Mtakatifu unapojifunza.
Utangulizi: Je, mara nyingine inaonekana kwamba Mungu si halisi? Au, kama yeye ni halisia, hajihusishi sana kuhusiana na sisi? Au, kama anajihusisha, anafanya mambo kwa sababu tusizozielewa? Yanapotokea haya, je, tunamlaumu nani? Maswali yote niliyoyauliza yanatoa shutuma kwa Mungu. Kutoa shutuma ni suala gumu ambalo kwa ujumla huwa linaendana na hoja za kweli. Lakini, mara zote tunapaswa tujiulize kuhusiana na mitazamo yetu tunapoamua kumshutumu/kumlaumu Mungu. Hebu tuzame kwenye somo letu la Biblia ili tujifunze zaidi kuhusu ukimbizi wa watu wa Mungu, mitazamo yao, na mtazamo tunaopaswa kuwa nao mbele za Mungu!
I. Utangulizi
A. Kumbuka kwamba tulijifunza jinsi Mfalme Daudi alivyokuwa akicheza kwa furaha alipoleta Sanduku la Agano la Mungu Yerusalemu (Samweli 6:12-15). Mwana wa Daudi, Mfalme Sulemani, alijenga Hekalu la Mungu Yerusalemu na akaliweka Sanduku la Agano Hekaluni (1 Wafalme 8). Hebu tusome sehemu ya sala/ombi la Mfalme Sulemani la kuliweka wakfu Hekalu na Sanduku la Agano. Soma 1 Wafalme 8:46-49. Je, Sulemani anaomba nini kuhusu dhambi na adhabu? (Anayaunganisha haya mambo mawili.)
1. Je, njia ya kuondokana na adhabu ni ipi? (Kumgeukia Mungu “kwa moyo wao wote.”)
B. Soma 1 Wafalme 8:59-61. Je, Sulemani anasema kuwa lengo la sala yake ni lipi? (Kwamba Mungu na watu Wake wawe na uhusiano ambao kila mtu anayeishi duniani ajue kwamba “Bwana ndiye Mungu na kwamba hakuna mwingine.”)
1. Je, hilo ndilo lengo maishani mwako?
II. Ibada ya Siri
A. Soma Ezekieli 8:1. Ezekieli anasema kwamba yupo nyumbani kwake na Wazee wa Yuda. Je, hiyo inamaanisha nini? (Lazima atakuwa alikuwa kwenye kikao fulani hivi cha kiutawala au cha kidini.)
1. Je, inamaanisha nini kwa kauli “mkono wa Bwana Mungu kumwangukia?” (Roho Mtakatifu anamtokea Ezekieli.)
B. Soma Ezekieli 8:2-4. Ezekieli anachukuliwa kwenye maono na Roho Mtakatifu. Je, maono yake yanamwelekeza wapi? (Kwenye mji mkuu, Yerusalemu, na kwenye lango la kaskazini la Hekalu – Hekalu lile lile lililowekwa wakfu na Sulemani kwa ajili ya utukufu wa Mungu.)
C. Soma Ezekieli 8:5-6. Je, watu wanauabudu wivu? (Hapana. Kutoka 20:5 inawaambia watu wasiabudu miungu ya uongo, kwa sababu Yehova ni “Mungu mwenye wivu.”)
1. Je, tunachukulia tu kuhusu mtu mmoja kuiabudu sanamu moja? (Hapana. Mungu anasema “Nyumba ya Israeli” inafanya mambo ya machukizo.)
2. Maelezo (“Commentary”) ya Keil na Delitzsch ya Agano la Kale inatuambia kuwa wanyama wa kafara walipelekwa kupitia kwenye hili lango ili waweze kutolewa kama kafara. Je, hii inapendekeza nini kuhusu asili ya hii dhambi? (Kwamba badala ya kumtegemea Mungu kwenye ibada yao, watu sasa walikuwa wanaitegemea miungu ya uongo.)
D. Soma Ezekieli 8:7-11. Ezekieli anaona kile kinachoendelea kwa kutoboa tundu kwenye ukuta wa hekalu. Je, unadhani hii ishara inamaanisha nini? (Hii sio ibada ya wazi. Ezekieli alikuwa anachungulia kupitia kwenye tundu alilolipanua hadi mlangoni. Hii ibada ilikuwa inafanyika nyuma ya milango iliyofungwa (au tuseme kwamba “nyuma ya pazia”).)
1. Soma Hesabu 11:16. Je, unadhani kuwa Ezekieli alikuwa akiwaangalia watu sabini? Au, je, unadhani kuwa neno “wazee sabibi” ni la kiishara? (Hesabu hii inaonekana kurejea watu sabini waliokuwa viongozi wa Israeli kipindi cha Safari ya Wana wa Israeli. Kwa hiyo, nadhani hii ni ishara ya uongozi wote wa taifa.)
E. Hebu fikiria kuhusu haya mafungu. Je, tunapaswa kuhitimisha nini kuhusu ibada ya Yuda katika kipindi chake? (Ezekieli ana kikao kikubwa baina yake na uongozi, na Mungu anamwonyesha kuwa wanaiabudu kwa siri miungu mingine. Lengo/Dhana nzima ya Hekalu imeharibiwa.)
1. Je, tunawezaje kutumia onyo hili hivi leo? Hata hivyo nina uhakika kuwa matendo yasiyo ya “siri” yanaendelea kanisani kwangu, lakini je, vipi kuhusu nyumbani mwetu? Je, tunaiabudu miungu mingine kupitia kwenye televisheni, intaneti, majarida au vitabu?
2. Je, tunaupotosha ujumbe wa kwamba Mungu wa kweli ndiye ambaye utukufu wote unamstahili?
F. Soma Ezekieli 8:12. Kwa nini watu wanamgeuka (wanampa kisogo) Mungu kisirisiri? (Aidha wanadhani Mungu hawajali (“Bwana ameiacha nchi”) au Mungu haelewi (Bwana hatuoni.”))
1. Je, watu wengine waliabudu miungu mingine kupitia kwenye televisheni, intaneti, majarida au vitabu kwa sababu walidhani Mungu hakuwajali au haelewi? Au, je, huku ni kufungamana kubaya – kwa dhati somo halijihusishi nasi sana hivi leo?
G. Hebu tupambanue asili ya tatizo kwa undani zaidi. Soma Ezekieli 8:16-18. Je, unadhani inamaanisha nini kulipa kisogo Hekalu na kuliabudu jua? (Walikuwa wanaiabudu asili. Walimpa kisogo Mungu wa kweli na badala yake kuabudu kile alichokiumba. Hii inabadili dhana nzima ya Hekalu na maana yake.)
1. “Kuliweka tawi puani” sio maneno niliyo na uzoefu nayo, ila nimewahi kusikia “kugeuza pua yako.” Je, ni kitu gani kingine wanakifanya hawa watu? (Wanawaumiza majirani wao na kuiabudu asili. Lengo la awali lilikuwa ni kumpa Mungu utukufu kupitia kwenye matendo mema ya watu.)
2. Je, Mungu anajibuje? (Mungu atatenda haki.)
III. Alama
A. Soma Ezekieli 9:1-2. Kundi la ajabu namna gani! Je, watu hawa ni akina nani? (Walinzi wenye silaha wa hekalu na mwandishi.)
B. Soma Ezekieli 9:3-4. Je, msingi wa kupata alama ni upi?
C. Soma Ezekieli 9:5-6. Tuafikiana kuwa tatizo la ibada lilienea kwa sababu wazee “sabini” walikuwa ni ishara ya uongozi mzima (wote). Je, kwa nini hukumu inaanzia hekaluni Yerusalemu? (Wale walikuwa waliokuwa katika uongozi. Wale waliokuwa karibu sana na mfumo wa ibada.)
1. Baini kiwango cha hukumu katika Ezekieli 9:4. Je, nani anayeepuka hukumu ya Mungu? (Wale “wanaougua na kulia kwa sababu ya machukizo yote yanayofanyika kati yake.”)
a. Je, hii inaendana na haki kwa imani? (Juma lililopita tulikubaliana kuwa haki kwa imani inaambatana na mtazamo sahihi. Wale walioepuka hukumu walifanya hivyo kwa sababu ya mtazamo wao. Walisumbuliwa na dhambi.)
(1) Je, hili ni somo linalohusika kwetu hivi leo? (Ndiyo. Tunaona kwamba watu walijihusisha kwenye uovu wa dhahiri, lakini ilipokuja suala la tutekelezwa hukumu, uamuzi uliugeukia mtazamo wao.)
D. Katika 2 Wafalme 25 Biblia inaandika uangamizi wa Babeli wa Hekalu lililojengwa na Mfalme Sulemani. Hekalu halikuleta tena utukufu kwa Mungu. Hukumu iliyoelezewa kabla na Ezekieli na watu wengine ilitekelezeka. Kumbuka watu walisema kwamba Mungu haelewi au hajali? Tunaona hapa kwamba Mungu alifahamu na kujali kwa sababu aliwaonya watu kuhusu hukumu, na kisha akaitekeleza. Hebu tugeukie mtazamo wa Mungu kuhusiana na hili.
IV. Mtazamo wa Mungu
A. Soma Yeremia 29:10-11. Tulichokisoma hivi punde katika Ezekieli kinaonekana kuwa cha kikatili. Je, mpango mkuu wa Mungu kwa ajili yetu ni upi? (Mungu anataka kutubariki, sio kutujeruhi. Hata na uangamizi wa Babeli wa Hekalu la Mungu, na mauaji na utekaji wa watu wa Mungu, Mungu anawaambia kuwa awataokoa katika kipindi cha miaka sabini.)
B. Soma Yeremia 29:12-14. Je, aina gani ya mtazamo Mungu anaitafuta hapa? (Anataka watu wake wamtafute kwa moyo wao wote.)
1. Soma tena Ezekieli 8:18. Je, nini kinacholeta utofauti kwenye utayari wa Mungu wa kusikiliza?
C. Je, ni uhusiano gani uliopo kati ya mtazamo wa “kuugua na kulia” wa Ezekieli 9:4, na mtazamo wa “kunitafuta na kuniona” wa Yeremia 29:13? (Kama lengo lako maishani ni kumpa Mungu utukufu kupitia kwenye uhusiano wako na Mungu, basi tatizo la dhambi Hekaluni litakuwa la kusumbua sana.)
V. Mwitikio wa Haki
A. Soma Nehemia 1:4-7. Nehemia aliposikia hukumu ya Mungu juu ya Yerusalemu, alifanya hii sala. Je, unadhani vitu gani vilivyo vya muhimu kwenye hii sehemu ya sala ya Nehemia? (Anamkiri Mungu wa kweli, aliye Mungu wa upendo. Anatubu dhambi.)
1. Je, unaweza kufikiria ombi ambalo Nehemia angekuwa akimshutumu Mungu kwa kuwa mzembe au asiyejali kwa sababu ya uangamivu wa hekalu na watu wa Mungu?
B. Hebu tuendelee na sala ya Nehemia. Soma Nehemia 1:8-9. Je, ni kitu gani katika sala/ombi tunakiona hapa? (Nehemia anakumbuka maelekezo ya Mungu na ahadi zake. Hebu baini lengo: “mahali nilipopachagua ili kuliweka jina langu hapo.” Utukufu wa Mungu ndilo lengo.)
C. Soma Nehemia 1:10-11. Je, Nehemia anajiweka kwenye nafasi gani kwa ajili yake katika sala yake? (Mwishoni!)
D. Je, unaweza kuona katika sala ya Nehemia, mtazamo wa “kuugua na kulia” na kitu cha “kunitafuta na kuniona?” (Ndiyo. Huu ni mchanganyiko wa ile mitazamo miwili ambayo Mungu anaitamania kwa ajili yetu.)
E. Rafiki, je, una mtazamo kama wa Nehemia? Je, hufurahii tatizo la dhambi? Je, unamtafuta Mungu kwa moyo wako wote kwa lengo la kumpatia utukufu? Kama sivyo, kwa nini usitubu leo na kumwomba Roho Mtakatifu abadilishe mtazamo wako?
VI. Juma Lijalo: Katika Roho na Kweli.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment