Somo limetafsiriwa na Mgune Masatu
(Wagalatia 6:11-18)
Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2011, Bruce N. Cameron, J.D. Marejeo yote ya maandiko yametoka kwenye tafsiri ya New International Version (NIV), copr. 1973, 1978, 1984 International Bible Society, isipokuwa kama itaelezwa vinginevyo. Nukuu kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya NIV inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji wa Biblia wa Zondervan. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Somo limekaa kimtazamo kwamba mwalimu anatumia ubao au sehemu nyingine yoyote ambayo inaweza kuonekana na wanafunzi. Kama huwa una kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na hukulipata kwa juma moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza pamoja na lugha nyingine kama vile Kifaransa, Kijerumani. Omba kwa ajili ya uongozi wa Roho Mtakatifu unapojifunza.
Utangulizi: Kama sote tunaye Yesu mmoja, ni kwa nini basi kuna haya makanisa mengi tofauti tofauti? Katika 1 Wakorintho 3 Paulo analalamika kuhusu mgawanyiko miongoni mwa waamini. Hivi leo inaonekana kuwa kila kanisa lina upekee muhimu kwake. Kwa mfano, Wabaptisti wana ubatizo kwa njia ya kuzamishwa majini. Ingawaje mimi sio Mbaptisti, nadhani hilo ni fundisho la muhimu sana. Je, ni kwa namna gani wale tulio na mafundisho ya kipekee tunapaswa kukabiliana na dunia? Je, Wabaptisti wanapaswa kuongoza kwa ubatizo kwa njia ya kuzamiswa majini? Je, kila dhehebu linapaswa kuongoza kwa imani yake ya kipekee (na ya kweli)? Katika hitimisho la ujumbe wa Paulo kwa Wagalatia, anatoa ushauri kwenye suala hili. Hebu tuzame kwenye somo letu la mwisho la Wagalatia na tuone kile tunachoweza kukigundua!
I. Uhalisia
A. Soma Wagalatia 6:11 na 1 Wakorintho 16:21. Je, hii inapendekeza nini kwako? (Kwamba kwa kawaida alimtumia mwandishi katika kuandika barua zake. Hata hivyo, binafsi angeweza kuandika sehemu ya barua yake ili kuthibitisha kuwa alikuwa mwandishi.)
A. Soma Wagalatia 4:15. Je, hii inapendekeza kuwa nini inaweza kuwa sababu ya uandishi wa maandishi makubwa wa Paulo kwa kutumia mkono? (Maoni mbalimbali yanapendekeza kuwa hii inathibitisha kwamba Paulo alikuwa na matatizo ya macho (kwamba alikuwa na uhafifu wa kuona vizuri).)
1. Je, ni kitu gani kingine kinachopendekezwa na maandishi makubwa? (Ilikuwa tu ni njia aliyokuwa akiitumia kuandika. Ninapokuwa ninatia saini mbele ya jina langu, saini yangu huwa ni kubwa. Ninapokuwa ninaandika, kwa ujumla huwa ninaandika maandishi makubwa ingawaje sina matatizo ya macho. Ama kwa hakika, katika uandishi, hali yangu ya macho ni bora zaidi kuliko watu wengine wenye umri kama wangu.)
1. Je, karatasi zenye ubora wa hali ya juu zilikuwepo kwa wingi? (Hatujui kile alichokuwa akikitumia kuandikia. Lakini, bila shaka kilikuwa ni cha gharama kubwa na kilipatikana kwa hali ya uchache. Huenda mwandishi kitaaluma aliandika maandishi madogo ili aweze kuwa na matumizi mazuri ya zana za kuandikia zilizokuwa na gharama kubwa.)
1. Kwa nini tunajihusisha (tunajali) sana na suala hili? Je, kuna umuhimu gani kwetu sisi kutokana na maoni ya Paulo kuhusiana na uandishi wake wa kutumia mkono? (Suala la kwanza tulilolijadili ndilo suala la msingi – kitabu cha Wagalatia kiliandikwa na Paulo. Tunaweza kuwa na uhakika na hilo.)
I. Hamasa ya Matendo/Wapinzani wa Sheria
A. Soma Wagalatia 6:12. Kama niliuza nguo kwa ajili ya kuendeleza maisha yangu, nadhani mara zote nitakuwa nikiangalia thamani za nguo za mtu ambaye nilikuwa nikizungumza naye. Kwa sababu mimi ni mwanasheria, vitu vingine vinanijia mawazoni, vinakuja vyenyewe tu pasipo kuamriwa: “Je, mtazamo wa mtu huyu katika kulisema hili ni upi?” “Je, mtu huyu anasema ukweli?” Kama mtu hana mtazamo wa kudanganya, kuna uwezekano mkubwa sana kuwa anasema ukweli. Hapa Paulo anafanya hoja ya kisheria kuhusu wapinzani wake. Kwa nini anahoji kuwa wapinzani wa matendo wanadanganya? (Ni watu wa kuwafurahisha watu tu. Hii ni sehemu tu ya juhudi zao kuepusha kujiingiza kwenye matatizo kwa sababu wao ni Wakristo.)
1. Nadhani ni busara kuendana na watu wanaotuzunguka. Kwangu mimi hiyo haionekani kuwa hoja kubwa. Je, kwa undani zaidi ni hoja gani unayoweza kuiona kwenye maneno ya Paulo? (Maoni kuhusu “msalaba” yanapendekeza kwamba wangeikana injili ili waweze kuwafurahisha/kuwapendeza wale wanaowazunguka. Tohara ni sehemu tu ya taswira kubwa ya kuikana injili.)
a. Je, unadhani kuwa hawa watu wanaowafurahisha watu watakubali “hatia” ya hili shtaka? Au, je, inawezekana kwamba hawakulifikiria hili kwa kina?
1. Juma hili nilikuwa ninasikiliza hubiri la mtu ambaye ni mwanafunzi wa dhati kabisa (makini) wa Biblia. Alikuwa anazungumza kuhusu unabii na jinsi ambavyo washiriki wa dini nyingine kubwa wataijia imani ya Yesu, hata kama wanaweza wasiwe na uelewa sahihi wa Utatu Mtakatifu. Hakujali sana kuhusiana na tatizo hili kwa sababu alisema, “Hakuna mtu hata mmoja aliye mkamilifu kwenye fundisho, lakini fundisho hili ni muhimu kiasi gani? (Kama huamini kuwa Yesu ni Mungu, huelewi sehemu ya msingi kabisa ya injili!)
A. Soma Wagalatia 6:13. Miaka nenda miaka rudi tunasoma kuhusu mashujaa wanaopokea vikombe kutoka kwa waathirika wao: ngozi za vichwa na nywele zake, masikio, nk. Je, Paulo anapendekeza kuwa kundi la waliotahiriwa linakusanya kitu gani? (Magovi!)
1. Je, kwa nini Paulo anakuwa mtu wa ishara sana? (Lazima atakuwa alikuwa anataka kuweka taswira nzuri kwa Wagalatia kwamba wapinzani wake kwa hakika kabisa hawakuwa wakiwajali.)
I. Mitazamo Sahihi
A. Soma Wagalatia 6:14. Je, Paulo anatofautianaje na watu wanaowafurahisha watu? (Wanaepuka kuteswa kwa ajili ya msalaba, anajivunia msalaba.)
1. Hebu tuliangalie hili kwa undani zaidi. Kwa nini wafurahisha watu wanajivunia kuhusu tohara na sio msalaba? (Wanajivunia vitu vitakavyowafanya waonekane wema mbele za macho ya watu wengine.)
1. Je, kanisa lako limetangaza? Washiriki wa kanisa la Mormon walikuwa na matangazo mazuri sana ya televisheni yanayohusu familia (kaya). Nimeona matangazo kama hayo ama kwa Walutheri au kwa Wamethodisti. Kanisa langu linajivunia kuhusu masuala ya afya na kuishi kwa muda mrefu kwa washiriki wake. Je, matangazo haya yanatangazwa ili kulifanya kanisa likubalike kwa jamii na kuepusha kuteswa?
a. Kanisa linapotangaza aina hii ya matangazo (nina uhakika makanisa mengi yanatangaza matangazo kama haya), je, tunajivunia kitu kingine kabisa tofauti na msalaba?
a. Je, Paulo anafanya ukosoaji wenye haki? Kwa mfano, je, Biblia inazungumzia kuhusu msalaba tu?
a. Kama nikikuuliza kuhusu shirika linaloitwa “Samaritan’s Purse,” je, utalielezeaje? (Makasha ya Krismasi kwa ajili ya watoto. Msaada wa majanga. Juma lililopita Franklin Graham, mkuu wa “Samaritan’s Purse,” alitembelea chuo kikuu ninachofundisha. Alisema kila walichokifanya kilikuwa ni kwa ajili ya kuiendeleza injili. Kujivunia kuhusu familia (kaya), afya, nk ni vema kama lengo lake ni kuiendeleza injili. Tatizo linakuja pale ambapo kujivuna kwetu kunaikana injili.)
a. Kabla hatujajisikia hatia kidogo, je, Paulo anamaanisha nini anaposema kuwa amesulibishwa kwa ulimwengu? (Hajali kile ambacho ulimwengu unakifikiria.)
(1) Je, tunapaswa kujali kile ambacho ulimwengu unakifikiria kuhusiana na kanisa letu?
A. Soma Wagalatia 6:15. Je, itakuwa vyema kusema kuwa “afya na urefu wa maisha” havina maana yoyote, kinachojalisha ni kuwa kiumbe kipya katika Kristo? (Afya na urefu wa maisha vina umuhimu wa kivitendo zaidi kuliko tohara, lakini kipindi kifupi cha maisha yetu hapa duniani hakina maana yoyote ikilinganishwa na umilele.)
1. Pale ambapo wafurahisha watu walipokuwa wakihoji wakiegemea upande wa tohara, je, walikuwa wakifanya hivyo kwa lengo la kuboresha maisha ya kila siku? (Hapana. Walikuwa wanahoji suala hilo kwa sababu za kiteolojia. Katika kitabu cha Mwanzo 17 Mungu alimwambia Ibrahimu kuwa tohara ilikuwa ni ishara kwamba palikuwepo na uhusiano kati ya Mungu na uzao wa Ibrahimu. Hiyo inaonekana kuwa na umuhimu mkubwa sana kwangu!)
1. Je, kuna kitu ambacho kanisa lako linahoji kuwa ni ishara maalum ya uhusiano kati yako na Mungu na ni cha muhimu sana kuliko msalaba?
A. Hebu turejee kwenye utangulizi wetu. Je, ubatizo kwa njia ya kuzamishwa majini ni muhimu sana kuliko msalaba? (Hapana.)
1. Je, tohara na ubatizo wa kuzamishwa majini vipo kwenye dhana moja? Je, Paulo hakuwa akihoji kwamba tohara ni kosa, wakati ambapo tunafahamu kuwa ubatizo ni kitu sahihi? (Tohara ni mbaya (makosa) tu kwa sababu ni sehemu ya njia ya matendo ya “tii na uishi,” badala ya njia ya neema ya “amini na uishi.”)
A. Hebu tuchunguze tena sehemu ya mwisho ya Wagalatia 6:15. Je, Paulo anamaanisha nini anaposema, “Kinachojalisha ni uumbwaji upya (yaani bali kimbe kipya)? (Soma 2 Wakorintho 5:17. Kinachojalisha ni kuwa kwa imani katika Yesu, tunaokolewa – tunakuwa kiumbe kipya.)
A. Hebu tusome 1 Wakorintho 7:19. Je, hii inafuta (inabatilisha) kila kitu tulichokijadili hivi punde? (Hapana! Tohara ilikuwa ni ishara ya uhusiano maalum na Mungu. Uhalisia wa uhusiano maalum na Mungu ni utii kwa amri zake. Tohara ilikuwa ni ishara. Utii ndio uhalisia.)
A. Je, kuna mtu anayeweza kuelezea kwa ufupi kile tulichojifunza? Au je, nimewachanganya ninyi nyote? Je, Wabaptisti wanapaswa kuongoza kwa ubatizo wa kuzamishwa majini? Je, kila kanisa linapaswa kuongoza kwa fundisho lake la kipekee? (Hapana. Tunapaswa kuongoza kwa msalaba – injili ya kuhesabiwa haki kwa neema pekee. Wakati huo huo, Wabaptisti (na wengine wote tuliosalia) tunapaswa kuendelea kutii amri za Mungu – huku tukitambua kuwa hatuokolewi kwa kuzitunza/kuzishika amri.)
A. Soma Wagalatia 6:16. Tukiuelewa vizuri uhusiano kati ya neema na matendo, je, nini kinachofuatia? (Amani na rehema!)
1. Je, mambo hayo mawili yanahusiana? (Rehema ya Mungu inanipatia amani. Inanipatia ujasiri kwenye wokovu wangu.)
A. Soma Wagalatia 6:17. Kwa nini tunaweza kuwa na uhakika na mafundisho ya Paulo? (Ameyasumbukia/ameyatesekea. Kwa wazi kabisa anayaamini.)
A. Soma Wagalatia 6:18. Tunamalizia kwa suala zuri ajabu linalozungumziwa kwenye Wagalatia – neema! Tunaokolewa kwa neema pekee.
A. Rafiki, kama haujaukubali wokovu kwa njia ya neema pekee hapo kabla, je, utaukubali sasa hivi? Je, utairuhusu rehema na amani viyaingie maisha yako?
I. Juma lijalo: Juma lijalo tutajifunza Utatu Mtakatifu tunapoanza mfululizo mpya wa masomo unaoitwa “Kumjua Mungu Wetu.”
Friday, December 23, 2011
Friday, December 16, 2011
Somo la 13: Injili na Kanisa
Somo limetafsiriwa na Mgune Masatu
(Wagalatia 6:1-10)
Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2011, Bruce N. Cameron, J.D. Marejeo yote ya maandiko yametoka kwenye tafsiri ya New International Version (NIV), copr. 1973, 1978, 1984 International Bible Society, isipokuwa kama itaelezwa vinginevyo. Nukuu kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya NIV inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji wa Biblia wa Zondervan. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Somo limekaa kimtazamo kwamba mwalimu anatumia ubao au sehemu nyingine yoyote ambayo inaweza kuonekana na wanafunzi. Kama huwa una kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na hukulipata kwa juma moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza pamoja na lugha nyingine kama vile Kifaransa, Kijerumani. Omba kwa ajili ya uongozi wa Roho Mtakatifu unapojifunza.
Utangulizi: Je, kanisa linapaswa kukabilianaje na dhambi? Je, juhudi za kanisa lako zimefanikiwaje katika kipindi cha nyuma? Mara nyingi, ninaona mambo mawili yakitokea. Kwanza, watu walio wakosoaji wanakosoa dhambi (au zinazodhaniwa kuwa ni dhambi) za watu wengine. Pili, wadhambi wanajisikia kuwa dhambi zao ni “mambo yao wenyewe’ na hivyo kuwataka viongozi wa kanisa “wajali mambo yao wenyewe’ – wakimaanisha kuwa, “tafadhali achana na mimi.” Waathirika wa ukosoaji wanafedheheshwa, na wadhambi waliokubuhu wanarejea ndani ya ganda lao la dhambi. Hebu tuzame kwenye somo letu la Biblia na tuone kile inachotufundisha kuhusiana na hii mada!
I. Mtego wa Dhambi
A. Soma Wagalatia 6:1. Je, inamaanisha nini “kunaswa” dhambini? (Dhambi yako inawekwa hadharani pale ambapo wewe mwenyewe hukupanga ijulikane hadharani. Au, ulijiingiza dhambini wakati ambapo ungependelea kutembea na Mungu.)
1. Je, hii inahusika kwa wadhambi majasiri? (Kama unajivunia dhambi zako, je, “umenaswa” nayo?)
B. Lazima kutakuwa na kosa la kiuchapaji kwenye Biblia yangu. Lazima Paulo atakuwa alimaanisha kuandika “nyie ambao ni wakosoaji mnapaswa kurejezwa,” sio “nyie ambao ni wa kiroho” mnapaswa kurejezwa. Je, hauoni zaidi hiyo ya awali kuliko hii ya pili?
1. Kama suala la “kiroho” pekee ndilo lilonapaswa “kurejezwa kwa upole,” je, hii inatufundisha nini kuhusiana na mfumo wa kanisa? Je, tunapaswa kuwazuia washiriki wetu walio wakosoaji wasikemee dhambi za watu wengine?
2. Fikiria nyakati ambazo ulikemewa aidha dhambi yako ya kweli au dhambi yako iliyofikiriwa tu lakini haikuwa dhambi. Je, ni viongozi wa kiroho wa kanisa walikukemea? (Mara nyingi huwa ni wageni na washiriki wapya wanaonikemea kwa sababu hawakubaliani na mawazo yangu! Mke wangu wa kiroho anafanya kazi nzuri sana ya kuniweka kwenye msitari sahihi!)
3. Unapoona dhambi kwa watu wengine, je, umegundua kuwa mara nyingi hiyo huwa ni dhambi yako uliyoigundua?
a. Je, kwa kukosa kwako vigezo, unapaswa kuondolewa kwenye mchakato wa “kuwarejeza” watu wengine wanaojihusisha na dhambi hizo hizo/zile zile zinazokufanya upambane nazo?
C. Je, inamaanisha nini kumrejeza mtu “kwa upole?” Je, hii inajumuisha kumfuta mtu ushirika wa kanisa?
1. Soma Mathayo 18:15-17. Je, Yesu anauelezeaje “upole?”
a. Utabaini kuwa katika mfano wa Yesu sio viongozi wa “kiroho” kanisani, bali ni mwathirika wa dhambi anayekabiliana na mdhambi. Je, unalinganishaje ushauri wa Paulo na ule wa Yesu?
II. Kuubeba/Kuuchukua Mzigo
A. Soma Wagalatia 6:2. Je, Paulo amebadili mada?
1. Je, dhambi ni mzigo maishani mwetu? (Ndiyo.)
2. Je, tunawajibika (kama tuna vigezo vya kiroho) kubeba mizigo ya dhambi za watu wengine?
3. Je, “sheria ya Kristo” ina nini cha kujihusisha katika kubeba mizigo ya dhambi za watu wengine? (Utakumbuka kwamba juma lililopita tulijadili tofauti kati ya njia ya“kuhesabiwa haki wa imani” kwenye maisha ya kila siku, na njia ya “matendo na sheria” kwenye maisha ya kila siku. Njia ya imani inauliza, “Je, ninaweza kufanya kitu gani ili nimpendeze Mungu, mwenzi wangu na wale wanaonizunguka hivi leo?” Njia ya matendo inauliza, “Je, ni alama gani nyekundu zinajielekeza kwenye dhambi nilizozivuka hivi leo?” Njia moja inajielekeza kwenye kuwapenda watu wengine, njia ya pili inajielekeza kwako wewe binafsi na kwenye dhambi. Njia ya imani, njia ya sheria ya Kristo, inauliza “Je, nifanye nini ili niweze kuchukua/kubeba mizigo ya watu wengine?” Hii itajumuisha kuwasaidia waushinde mzigo wa dhambi.)
B. Je, ni umuhimu gani unaouhusianishwa na neno “kubeba?” (Kubeba kunaonekana kumaanisha zaidi tu ya msaada mdogo.)
1. Je, ninawezaje “kubeba/kuchukua” dhambi ya mtu mwingine? (Je, ni mara ngapi dhambi ya watu wengine inakuathiri vibaya sana? “Kubeba/kuchuhua” dhambi wakati unamrejeza mtu inamaanisha kuwa unaweza kuwa unateseka kutokana na dhambi ya mtu huyo.)
III. Majivuno Katika Ubebaji/Uchukuaji wa Mzigo
A. Hebu turudie tena kusoma sehemu ya mwisho ya Wagalatia 6:1. Chukulia kwamba unamsaidia mshiriki mwenzako wa kanisa aliyeelemewa na usemaji wa uongo. Je, Paulo anatuambia kuwa kama tukimsaidia mshiriki kama huyo, yumkini nasi tukaanza kuwa waongo?
B. Soma Wagalatia 6:3-5. Hivi punde tu Paulo ameniambia kuchukua/kubeba mizigo ya watu wengine. Sasa ananiambia kuwa nibebe furushi langu mwenyewe!
1. Je, ushauri wa Paulo ya kwamba tuwe waangalifu kuhusu kutojaribiwa unahusika hapa? (Vipande vya fumbo/kitendawili vinaungana! Kama tunamsaidia mwongo na dhambi yake, tunaweza kujaribiwa na majivuno na kudhani kuwa sisi ni wa hadhi ya juu. Tunaweza kujaribiwa kwa usengenyaji kwa kuwaambia watu wengine jinsi gani mtu fulani alivyo mtu mbaya. Tunahitajika “kubeba/kuchukua” mizigo yetu ya majivuno na usengenyaji.)
2. Paulo anatuambia kuwa “tuzipime kazi zetu wenyewe,” “acha majivuno,” na tuachane na masuala ya “kujilinganisha” na watu wengine. Je, anatuambia kuwa tufanye kitu gani? (Hatuwezi kujilinganisha na mwongo. Hatuwezi kuwa na majivuno kutokana na ukweli kwamba sisi sio waongo. Hatupaswi kupima kwa kutumia kipimo cha juu sana “wema” wetu. Tunapaswa kujilinganisha na Yesu, sio na watu wengine. Kumfanya Yesu kuwa kituo cha ulinganifu, kuwa makini na dhambi yetu weyewe, ni “kubeba/kuchukua” “furushi letu” wenyewe.)
C. Sasa basi tumekwishajadili mada hii, je, ni vigezo gani ambavyo kanisa linapaswa kuvitumia kwa “wanawaorejeza” wale walionaswa dhambini? (Hawa wanapaswa kuwa watakatifu wanyenyekevu walio na ufahamu/utambuzi wa dhambi zao wenyewe, wasio wasengeyaji, na walio wapole kwa sababu wanatambua kuwa Mungu amekuwa na upole na unyenyekevu kwao.)
IV. Wakufunzi Wenye Mbaraka
A. Soma Wagalatia 6:6. Hapa ndipo utakaponikaribisha chakula cha usiku! (Hapa anamaanisha kumtoa mtu out – yaani kumpa ofa! Zingatia: Mwandishi huyu ni Mhadhiri (Profesa)). – mkazo (emphasis) ni wangu.
1. Je, ushauri huu unaelekezwa kwa nani? (Paulo anazungumza na wale walionaswa dhambini ambao wamefaidika kutokana na wale wanaowarejeza kwa upole na kubeba/kuchukua mizigo yao.)
a. Je, wadhambi waliorejezwa wanapaswa kufanya nini? (Wanapaswa kuwa mbaraka kwa wale waliowarejeza.)
b. Je, umewahi kuhusika katika kumrejeza mdhambi na kuishia kupata adhabu kutokana na urejezaji huo? (Miaka mingi iliyopita, wenzi fulani waliniomba kuwasaidia kwa sababu walikuwa wakipitia wakati mgumu sana kwenye ndoa yao. Dhambi ilihusika. Nilikutana nao, na nikajitolea kuwa yeyote kati yao aishi nyumbani kwangu kwa muda hadi hapo ambapo wangeweza kuishi pamoja tena. Ilitokea kuwa nilishutumiwa kwa “kufungamana” na mwenzi aliyekuja kuishi nyumbani kwangu kwa muda – ingawaje wenza hao walikubaliana wao wenyewe kuwa nani aje kuishi nasi (mimi pamoja na mke wangu!))
V. Malipo
A. Soma Wagalatia 6:7-8. Kwa nini Paulo anamrejea Mungu kudhihakiwa kwenye sheria ya malipo? (Kama Mungu ndiye mmiliki wa dunia, basi tunapaswa kuwa na uwezo wa kuzitegemea kanuni fulani fulani. Mojawapo ya kanuni hizi ni kanuni ya “malipo.” Kutafuta kuwasaidia watu wengine kunaleta msaada kwako. Kuwadhuru watu wengine kunaleta madhara kwako.)
1. Je, hii inahusianaje na wazo la kumrejeza mtu aliyenaswa dhambini? (Inakupa hoja kwenye jaribu lako la kurejesha! Lakini, wazo la msingi ni kwamba kuonyesha upendo na wema kwa watu wengine kutatupa thawabu.)
B. Soma Wagalatia 6:9. Je, kwa nini tunaonywa kuhusu “kuchoka?” (Ingawaje Mungu yupo kwenye umiliki, dhambi na uhuru wa uchaguzi vinatawala. Mara nyingine malipo yanacheleweshwa. Mara nyingine hatutapewa malipo hadi tutakapofika mbinguni.)
1. Kwenye somo letu la Wagalatia, tumenyumbulisha umuhimu wa “neema.” Je, huu mfululizo wa mafungu unatufundisha nini kuhusu umuhimu wa matendo? (Neema inatupatia wokovu, lakini matendo yana thawabu – thawabu chanya na hasi. Paulo anataja kwa mahsusi thawabu inayotusubiri mbinguni kutokana na matendo yetu mema!)
C. Angalia tena Wagalatia 6:8. Je, nini kilicho cha muhimu kuhusu njia ambayo Paulo anaelezea upandaji sahihi? (Hebu baini njia ya neema: kupanda “kwa kumpendeza Roho.” Utume wetu ni kumpenda Mungu na kuwapenda wale wanaotuzunguka.)
D. Soma Wagalatia 6:10. Kwa nini Paulo anatofautisha kati ya jamaa ya waaminio na watu wengine? (Tuna wajibu mkubwa kwa wale wanaoamini.)
E. Rafiki, je, utaliweka lengo lako ili uwe wa kiroho zaidi ili kwamba uweze kusaidia kubeba/kuchukua mzigo wa dhambi wa watu wengine? Kama umetambua kuwa wewe u mkosoaji zaidi kuliko mtu wa kiroho, je, utamwomba Roho Mtakatifu akusaidie utoke kwenye ukosoaji hadi kuwa mtu wa kiroho?
VI. Juma lijalo: Kujivunia Msalaba.

Friday, December 9, 2011
Somo la 12: Kuishi kwa Kuongozwa na Roho Mtakatifu
Somo limetafsiriwa na Mgune Masatu
(Wagalatia 5:16-25)
Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2011, Bruce N. Cameron, J.D. Marejeo yote ya maandiko yametoka kwenye tafsiri ya New International Version (NIV), copr. 1973, 1978, 1984 International Bible Society, isipokuwa kama itaelezwa vinginevyo. Nukuu kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya NIV inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji wa Biblia wa Zondervan. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Somo limekaa kimtazamo kwamba mwalimu anatumia ubao au sehemu nyingine yoyote ambayo inaweza kuonekana na wanafunzi. Kama huwa una kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na hukulipata kwa juma moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza pamoja na lugha nyingine kama vile Kifaransa, Kijerumani. Omba kwa ajili ya uongozi wa Roho Mtakatifu unapojifunza.
Utangulizi: Hakuna Mkristo mkomavu anayeamini kwamba imani ndio jibu la mwisho la “ni kwa jinsi gani tunapaswa kuishi?” Kufikiri na kutenda vinaendana. Hakuna Mkristo wa dhati anatakayedai kuwa kutembea na Mungu ni jambo rahisi. Wakristo wengi ninaowafahamu kimsingi wanasema, “Ninaokolewa kwa neema pekee. Kwa sababu ya upendo wangu kwa Mungu, ninafanya uamuzi wa kutembea nae na kuyafanya/kuyatenda mapenzi yake.” Nilipojaribu kuwauliza zaidi waliongezea kwa kusema, “Na, kama mtu hatembei pamoja na Mungu, hiyo inaonyesha kuwa hawana imani.” Ama kwa hakika, wale “Wakristo” wanaotumia imani kama kisingizio cha kuishi maisha ya kiovu hawaielewi injili. Lakini, baadaye, nimekuwa nikilitafakari zaidi suala hili kuhusiana na jinsi gani Mkristo anayeokolewa kwa neema anavyopaswa kuenenda katika maisha yake ya kila siku. Hebu tuzame kwenye Biblia yetu na kuona kile ambacho Paulo anatufundisha kuhusiana na maisha ya kila siku!
I. Mzozano/Ugomvi
A. Tunahitaji kupata muktadha, kwa hiyo kwanza kabisa hebu soma kwa haraka Wagalatia 5:16-21. Je, hii inatuambia nini kuhusu neema na kuishi maisha sahihi? (Kama unaishi maisha yenye ubinafsi, maovu, yasiyo makamilifu, hutakwenda mbinguni.)
1. Huyu ni Paulo anayeandika haya! Je, hii inatenda kitu gani kwenye fikra zetu kuhusu neema? (Inamaanisha kuwa mwisho wa neema hauwezi kuwa ni tabia ya kiovu.)
2. Majuma mawili yaliyopita tulijifunza kuwa “mchakato” wa Sara kutimiza lengo la Mungu (kwamba Ibrahim atakuwa na uzao) uliishia kwenye balaa kubwa sana. Je, hakuna tunachoweza kukifanya (au tunapaswa kukifanya) ili tujihusishe kwenye kuishi maisha sahihi? Je, hilo litakuwa ni “mpango wa Sara,” yaani, kosa la “kuhesabiwa haki kwa matendo?”
B. Hebu tuyaangalie haya mafungu kwa undani zaidi. Soma Wagalatia 5:16. Je, inamaanisha nini “kuishi kwa kuongozwa na Roho?” (Ishi kwa mujibu wa uongozi wa Roho Mtakatifu.)
C. Soma Wagalatia 5:17. Je, hili suala la kuishi kwa kuongozwa na Roho linatendeka?
1. Kama umesema kuwa, “Ndiyo,” je, unaielezeaje kauli ya Paulo kwamba “hamfanyi yale mnayoyataka?” (Inaweza kumaanisha kuwa mnataka kufanya jambo jema, lakini badala yake mnafanya uovu. Pia inaweza kumaanisha mna matamanio ya asili ya kutenda uovu, lakini kwa sababu ya Roho Mtakatifu, badala yake mnatenda jambo jema. Hii maana ya pili inaendana na kile tulichokisoma hivi punde katika fungu la 16.)
a. Soma Warumi 7:21-25. Je, Paulo anazungumzia tu kuhusu watu wabaya? Au, je, anamzungumzia tu wewe na mimi? (Paulo anajizungumzia yeye mwenyewe. Anazungumzia kuhusu Wakristo “wazuri.” Sote tuna asili ya dhambi. Sote tunavutwa kuishi kwa mujibu wa asili hiyo. Tunajikuta tunatenda uovu ambao hatutaki kuufanya.)
D. Soma Wagalatia 5:18. Je, hii inamaanisha nini – sina haja ya kuwa na wasiwasi juu ya kile ambacho sheria inakisema? (Haiwezi kumaanisha hivyo, kwani hivi punde tu umesoma kuwa watenda maovu hawatakwenda mbinguni. Hitimisho la pekee la kimantiki ninaloweza kulifikia ni kuwa tuna chaguzi mbili. Tunaweza kuongozwa na Roho Mtakatifu au tunaweza kuongozwa na asili yetu ya dhambi.)
1. Je, hii inapendekeza kuwa kwa namna fulani hivi sheria inahusianishwa na asili yetu ya dhambi? (Soma Warumi 7:8-10. Paulo anasema kuwa sheria inachokonoa tabia ya kidhambi. Hii sio ya kawaida, kwa hiyo tunahitajika kulichunguza hili zaidi.)
II. Kuishi kwa mujibu wa Sheria
A. Sijui jinsi ya kuwa na mjadala thabiti wa hili suala bila kuzungumzia dhambi mahsusi. Kwa hiyo, hebu tuzungumzie kuhusu kisa mahsusi kuhusiana na dhambi mahsusi. Soma 2 Samweli 11:1-4. Nimefundisha kisa hiki mara nyingi, nimehubiri kuhusiana nacho. Kama wewe ndiye ungekuwa Daudi, na ukataka kuepuka hii dhambi, je, ni hatua gani za kivitendo ambazo ungezichukua? (Kile ambacho mara zote nimekuwa nikikisema huko nyuma ni kwamba Daudi alikuwa anachukua mfululizo wa hatua kuelekea kwenye dhambi. Baadhi ya hatua zinaweza zisiwe dhambi, lakini bado zilimwelekeza kwenye uelekeo wa dhambi.)
1. Je, hizi hatua mbaya zinaweza kuwa zipi? (a. Kutokwenda vitani na majeshi yake; b. Kumwangalia Bathsheba kwa muda mrefu; c. Kuvutiwa/kupendezewa nae; d. Kutuma apelekewe hata ingawaje alijua kuwa alikuwa ameolewa; na hatimaye kufikia ukomo wa dhambi, e. Kufanya uzinzi.)
2. Kama wewe (namaanisha wewe binafsi) ulitaka kuepuka uzinzi, je, ungeepuka kuchukua hizi hatua? (Ndiyo. Hii inaleta mantiki. Lakini, nadhani kwamba nimekuwa nikifundisha kwa kutumia njia isiyo sahihi. Kiini cha hatua ni sheria. Kiini cha hatua ni uzinzi na jinsi ya kutousogelea kwa ukaribu sana. Kuilenga dhambi na sheria ni njia ya kuhesabiwa haki kwa matendo.” Ninaiangalia asili yangu ya dhambi na ninatafakari jinsi ya kuishinda. Kama Sara, mimi ni mhandisi wa nini cha kufanywa ili kutimiza lengo la Mungu.)
3. Je, onyo la kivitendo la Paulo kuhusu kuhesabiwa haki kwa imani ni lipi? (Halifanyi kazi. Katika Warumi 7:5 Paulo anasema kuwa sheria inaamsha matamanio yetu ya kidhambi. Wagalatia 5:3 inapendekeza kuwa haiwezekani kuitimiza sheria. Katika Wagalatia 5:4 Paulo anaeleza kuwa njia ya matendo inashindwa kwa sababu inamwondoa Mungu kutoka kwenye mpambano.)
4. Je, kuna chochote tunachoweza kukifanya ili kuendeleza tabia zetu wenyewe? Hebu tubaini hilo katika sehemu inayofuatia.
III. Kuishi kwa mujibu wa Roho
A. Soma Wagalatia 5:22-23. Je, ni kwa jinsi gani kuishi kwa mujibu wa Roho kunatofautiana na kuishi kwa mujibu wa sheria? (Unazingatia masuala chanya, hauzingatii masuala hasi. Hauelekezi hatua zako kuelekea dhambini, unaelekeza hatua zako kuelekea kwenye haki.)
1. Hebu turejee kwenye mfano wetu wa msingi wa Daudi. Kama umeamua kuacha kuwafundisha akina Daudi wa siku zijazo kuziangalia hatua zao, kuacha kuziangalia “taa nyekundu” za kimaadili, sasa utakuwa unawafundisha kitu gani? (Vipi kama badala yake tungesema “Mtizamie/mwangalie mkeo. Leta upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, upole na kiasi kwenye maisha ya mkeo. Usiziangalie ‘taa nyekundu.’”)
B. Hebu turejee tena kitu fulani tulichojadili juma lililopita. Soma Wagalatia 5:14-15. Hili ndilo lengo la maisha yanayoongozwa na Roho. Je, Daudi angepaswa kuwa anajiuliza kuhusu kitu gani, badala ya kuuliza “Ni hatua gani za kuielekea dhambi (Bathsheba) ninazopaswa kuziepuka?” (Je, ninaweza kufanya jambo gani ili niweze kumfurahisha mke wangu? Je, ninaweza kufanya jambo gani ili niweze kumfurahisha Mungu wangu? Je, ninaweza kufanya jambo gani ili niweze kumsaidia mke wangu? Je, jukumu hili linapendeza mbele za Mungu wangu na mke wangu?
1. Je, hii inakusaidia kuelewa kile anachokimaanisha Paulo anapoandika “kama unaongozwa na Roho, haupo chini ya sheria?” (Roho anauliza, “je, nifanye nini ili niweze kumpenda Mungu na mwenzi wangu?” Sheria inasema, “Je, ninapaswa kufanya nini ili niweze kuuepuka uzinzi?” Lengo ni lile lile – kuwa mwaminifu kwa mwenzi wako. Kama vile Sara na Mungu walivyokuwa na lengo moja – kuwapata wazao kwa ajili ya Ibrahim. Ni mchakato, njia ya kulielekea lengo, linalowatenganisha wale wanaoamini katika kuhesabiwa haki kwa imani na wale wanaoamini katika kuhesabiwa haki kwa matendo.)
2. Wagalatia 5:13 inapotualika “kuwatumikia” wengine, na Wagalatia 5:22 inapotuambia kuwa tunda la kwanza la kuishi maisha yanayoongozwa na Roho ni “upendo,” je, hii inatuambia nini kuhusu kujitazamia wenyewe, ubinafsi, “kutizama kitovu?” (Mambo haya ni makosa.)
a. Je, kuna funzo katika jambo hili kwa ajili yetu kuhusu jinsi ambavyo tunapaswa kutembea na Mungu? (Rafiki, natumaini kwamba unaweza kuona kuwa kuitazamia sheria, kuzitazamia “taa nyekundu” ni kujitazamia mwenyewe. Je, ninaendeleaje? Kutazamia kumpenda Mungu na wenzi wetu na wengine kunafikia kwenye swali, “Je, vinaendeleaje? Je, ninavifurahisha?)
C. Soma Wagalatia 5:24. Je, njia yetu ya kukabiliana na asili yetu ya dhambi inapaswa kuwa ipi? (Tunataka ife! Je, unaweza kuona tena kuwa ni makosa kwa kiasi gani kuzitazamia asili zetu za dhambi na kupima vipimo vyake kuielekea dhambi?)
D. Soma Wagalatia 5:25. Kama unataka kuendana hatua kwa hatua na mwanadamu mwingine, je, unahitajika kufanya nini? (Angalia jinsi mtu huyo alivyotembea.)
1. Je, inamaanisha nini kuendana “hatua kwa hatua” na Roho? (Kumwangalia Mungu wetu na kile kinachompendeza.)
2. Hebu turejee tena Wagalatia 5:24-25. Je, sheria bado ni ya muhimu? (Ndiyo. Kama Wakristo “wasio wakomavu” sheria inatufundisha kuwa tunamhitaji Mwokozi. Lakini, mara tunapoupata huo ujumbe, basi hatupo tena chini ya uangalizi wa sheria. Hatujiangalii tena sisi wenyewe, kujipima wenyewe dhidi ya sheria. Badala yake, tunamwangalia Mungu, huku tukiwa tukiongozwa na Roho Mtakatifu wa Mungu ili tuweze kumpendeza Mungu. Basi kinachomiminwa maishani mwetu ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, upole na kiasi.)
a. Kama unajiona kuwa wewe sio mvumilivu, je, unapaswa kulifanyia hilo kazi? (Hapana! Hauiangalii dhambi. Usiyaangalie matendo, na kwa ujumla kuenenda kama Sara alivyofanya. Kwa uwezo wa Roho wa Mungu, badala yake zingatia kumpenda mtu ambaye huna uvumilivu nae. Hiyo ndio njia ya neema. Hiyo ndio njia ya kuhesabiwa haki kwa imani.)
E. Soma Wagalatia 5:26. Kwa nini tuwe na majivuno kwa kuishi maisha sahihi? (Kama lengo ni kwa jinsi gani tunaishinda dhambi, na kama hatuko macho sana, hili linaweza kutokea. Kama lengo letu ni kumpenda Mungu na wale wanaotuzunguka, kamwe hili haliwezi kutokea.)
F. Rafiki, natumaini kwa sasa unaweza kuona kwamba haki kwa imani sio tu kuwa inatuokoa kwa neema ya Mungu, bali pia inatuambia jinsi ambavyo tunapaswa kuishi kila siku. Je, utaamua hivi sasa kuacha kuangalia na kuzitazamia “taa nyekundu” na kuanza kuangalia jinsi ya kumpenda na kumfurahisha Mungu?
IV. Juma lijalo: Injili na Kanisa.

Friday, December 2, 2011
Somo la 11: Uhuru Katika Kristo
Somo limetafsiriwa na Mgune MAsatu
(Wagalatia 4:1-15)
Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2011, Bruce N. Cameron, J.D. Marejeo yote ya maandiko yametoka kwenye tafsiri ya New International Version (NIV), copr. 1973, 1978, 1984 International Bible Society, isipokuwa kama itaelezwa vinginevyo. Nukuu kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya NIV inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji wa Biblia wa Zondervan. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Somo limekaa kimtazamo kwamba mwalimu anatumia ubao au sehemu nyingine yoyote ambayo inaweza kuonekana na wanafunzi. Kama huwa una kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na hukulipata kwa juma moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza pamoja na lugha nyingine kama vile Kifaransa, Kijerumani. Omba kwa ajili ya uongozi wa Roho Mtakatifu unapojifunza.
Utangulizi: Uhuru ni kitu kizuri sana! Sote tunafahamu kuwa tunataka kuwa huru. Tunakuwa tunafahamu pale ambapo tunakuwa hatuna uhuru. Lakini je, hivi maana ya uhuru ni ipi hasa? Naweza kuwa na uhuru wa kumpiga ngumi puani jirani yangu. Lakini, hatadhani kwamba alikuwa huru kama angekuwa anapigwa ngumi na mimi mara kwa mara! Je, Paulo anamaanisha nini anapotuambia “kusimama imara” katika uhuru wetu? Hebu tuzame kwenye somo letu la Wagalatia na kuona kile tunachoweza kujifunza!
I. Simama Imara
A. Soma Wagalatia 5:1. Je, ni nani aliyetupatia uhuru? (Yesu.)
1. Unapomchukulia mwanzilishi wa uhuru wetu, je, hiyo inatuambia kitu fulani kuhusiana na asili ya uhuru wetu? Kwa mfano, je, Yesu angetupatia uhuru wa kuwadhuru wengine?
2. Je, tuko huru na kitu gani? (Paulo anatuambia kuwa “mzigo” wa “kongwa la utumwa” umebebwa.)
B. Soma Wagalatia 5:2-4. Je, hili kongwa la utumwa ni kitu gani? (Paulo anataja tohara, lakini pia anataja “torati yote.”)
1. Kama sheria ni nakala ya tabia ya Mungu, kama ambavyo nimesikia mara kwa mara, je, yawezaje kuwa kongwa la utumwa? (Sidhani kama sheria/torati ndio “kongwa,” badala yake nadhani ni matakwa yanayotakiwa, kwamba tuitimize torati yote (tuishike sheria yote) ama tufe, hilo ndilo kongwa la utumwa. Ni kazi kubwa kutimiza kile kisichowezekana. Ni kama “Sisyphus” kusukuma mwamba kuelekea juu ya kilima.)
Muhimu: “Sisyphus” ni mungu wa Kigiriki. Alihukumiwa kusukuma jiwe kubwa juu ya kilima maisha yake yote. Jiwe lenyewe ni kubwa kiasi kwamba hata haliwezi kuvingirika, lakini pamoja na yote hayo bado anapaswa kulisukuma ili liweze kwenda juu ya kilima.
2. Paulo anaposema, “Sikilizeni maneno yangu,” je, unadhani anasema kitu gani? (Hili ni jambo la muhimu!)
3. Je, kuhesabiwa haki kwa matendo ni “upinga Kristo?” (Ndiyo. Ndio maana mazungumzo haya ni ya muhimu sana. Kama unaamini kwamba matendo yako ni ya msingi sana kwa ajili ya wokovu wako, basi umemtupilia mbali Yesu na matendo yako yamechukua nafasi yake. Wewe ni mpinga Kristo.)
4. Je, hakuna upande fulani hivi wa kati – kwamba ninaamini katika wokovu kwa imani lakini pia ninaamini kwamba matendo mema ni muhimu kwa ajili ya wokovu wangu? (Kama tunadhani kwamba matendo yetu yanatuhesabia haki, basi “tunatengwa” na Yesu. Hatuwezi kuidai neema kwa sababu “tumetanga mbali na neema.”)
II. Utafakari Uhuru
A. Soma Wagalatia 5:5-6. Kama kuhesabiwa haki kwa matendo kunapaswa kuepukwa, je, tunapaswa kutafuta kitu gani? (Roho Mtakatifu. Roho Mtakatifu ndiye wakala wa kutupatia haki.)
1. Je, imani ni suala tu la utamkaji? (Paulo anarejea suala la “imani kujielezea yenyewe kupitia upendo.” Ni zaidi ya utamkaji tu.)
B. Hili wazo la kuielezea imani yetu kupitia kwenye upendo linatuelekeza nyuma kwenye mjadala wetu kuhusu kile ambacho uhuru unamaanisha. Kama kweli ungekuwa huru, ungeweza kufanya jambo lolote, sawa? Hebu turukie mbele kidogo. Soma Wagalatia 5:19-21. Kama kweli ungekuwa huru, ungekuwa na uwezo wa kutenda mambo haya, sawa? (Paulo anatuambia kwamba hatuwezi kuyafanya mambo haya halafu tuurithi Ufalme wa Mungu. Lazima Paulo atakuwa na maana nyingine ya uhuru.)
C. Fikiria maelezo fulani. Chukulia kwamba una mtoto mwenye umri wa miaka miwili. Halafu unamwambia mwanao, “ninakupa uhuru. Unaweza kufanya chochote utakacho. Lakini, kama unataka mwendelezo wa malezi na msaada wangu, basi unapaswa kushi nami na kufuata maelekezo yangu.” Kama wewe ndiye mtoto mwenye miaka miwili, njia yako ya uhuru itakuwa ipi? (Utakufa kama utachagua kuenenda njia zako mwenyewe. Kuwa mfu ndio mwisho wa uhuru wako wa kufanya uchaguzi. Njia pekee ya kuendelea kuishi ni kumchagua mzazi wako. Yesu alitupatia fursa ya uhuru wa mauti ya milele. Lakini, uhuru wa kweli unatutaka tutembee naye.)
D. Hebu tuliangalie hili katika mtazamo mwingine. Je, ni uhuru wa aina gani unaotaka kuufurahia mbinguni? Je, ungependa wananchi wenzako kule mbinguni waweze kufurahia “chuki, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi, husuda, ulevi na ulafi?” (Kama chanzo na mateso hapa duniani kitajipenyeza na kuingia kule mbinguni, basi hutaufurahia uhuru.)
E. Mfano wa mwisho kabisa. Fikiria dhambi uliyoifanya ambayo unaijutia kabisa kuliko zote. Je, “ulifurahia” uhuru kwenye hiyo dhambi? (Kwa wazi kabisa, ulikuwa huru kuitenda dhambi, lakini kilichofuatia ni mateso! Rafiki, tunaweza kuangalia uzoefu wetu wenyewe ili tuweze kuelewa kwamba njia pekee ya kuufurahia uhuru wa uchaguzi ni kufanya maamuzi sahihi.)
III. Uhuru na Upendo
A. Soma Wagalatia 5:13-14. Je, hilo umelisikia wapi hapo kabla? (Unaweza kushangazwa kwa kutambua kwamba umelisikia zaidi ya mara moja! Soma Mambo ya Walawi 19:18 na Mathayo 22:37-40.)
1. Je, uhuru niliopewa na Yesu unamaanisha kuwa sina wajibu? (Hapana! Inamaanisha kuwa nina wajibu wa kuwapenda wengine kama ninavyojipenda mwenyewe na wajibu wa kuepuka kutosheleza matamanio ya asili yangu ya dhambi.
B. Je, kauli ya Paulo inaendana na mjadala wetu wa kile tunachokidhani ni uhuru wa kweli? (Hatuambii kitu ambacho ni kipya kwenye uzoefu wetu wenyewe.)
1. Je, tunakubaliana kuwa tunapomdhuru mtu mwingine basi tunajidhuru wenyewe? Na, tunapompenda mtu mwingine, basi tunajipenda wenyewe?
C. Soma Wagalatia 5:15. Je, hii inatuambia nini ambacho tayari tunakijua kuhusu kuwadhuru watu wengine kwa “uhuru” wetu? (Wanalipiza kisasi! Watachukua kipande kutoka mafichoni mwako!)
IV. Wakili wa Upande wa Pili
A. Tumekuwa tukirukia rukia mafungu kwenye Wagalatia 5, hebu turejee nyuma na kusoma mafungu tuliyoyaruka. Soma Wagalatia 5:7. Hii ni njia isiyo ya kawaida ya kuelezea kuhesabiwa haki kwa imani: kuuheshimu ukweli! Au, ndivyo hivyo? (Sio njia isiyo ya kawaida. Uamuzi wa kumwamini Mungu na kumtumainia Mungu (kama ilivyokuwa kwa Ibrahimu) ni sawa kama vile uamuzi wa mtoto wa miaka miwili wa kuwatii na kuwatumainia wazazi wake. Ni uamuzi kuhusu kiapo cha utii.)
B. Soma Wagalatia 5:8. Nani anayeweza kuondosha kama mwanzilishi wa kuhesabiwa haki kwa imani? (Yesu.)
C. Soma Wagalatia 5:9. Je, ni vigumu kiasi gani kukabiliana na kosa/dosari? (Hii ni enye kudhuru kwa siri! Inajipenyeza na kuambukiza kanisa zima.)
D. Soma Wagalatia 5:10. Je, tunaweza kukubaliana na Paulo? Kutokana na kile alichokiandika hadi hivi sasa, kwa nini awe jasiri kiasi hicho?
1. Kama tuna aina fulani hivi ya wazo “jipya” la kulitikisa kanisa, je, tuchukulie jambo gani? (Kama wazo letu halina msingi wa Biblia, kama tunaleta mikanganyiko kanisani, basi tutalipa adhabu.)
a. Je, tunamfahamu anayesababisha mikanganyiko? (Shetani. Paulo anatuambia kuwa hawezi kuwa Yesu. Kwa hiyo, lazima atakuwa ni –
b. mpinzani wa Yesu (Shetani) na wafuasi wake wanaofanya mambo haya kanisani.)
E. Hebu ruka mbele kidogo na usome Wagalatia 5:12. Kwa ulinganisho, soma tena Wagalatia 5:6. Je, unazilinganishaje hizi kauli mbili? (Kosa la msingi linahitaji jibu madhubuti.)
F. Soma Wagalatia 5:11. Kwa nini kosa la kuhesabiwa haki kwa matendo ni “kosa la msingi?” (Linabatilisha msalaba. Mungu wetu alisulubiwa. Wazo la mungu kusulubiwa ni “kosa/hatia.” Nani ambaye atamfuata mungu aliyeuawa? Tunafanya hivyo! Wakristo wanaelewa kwamba maisha, kifo na ufufuo wa Mungu wetu ndio ufunguo wa uzima wetu wa milele. Kama hulipati suala hili kwa usawia, basi wewe sio Mkristo.)
G. Rafiki, je, unaipata hoja ya Paulo inayosema kwamba njia ya Mungu ya kuuelekea uhuru wa kweli ni kuamini, kumtumaini na kumheshimu yeye. Tunaokolewa kwa neema, kwa kumchagua Yesu, lakini haya sio maneno tu, ni uchaguzi wa maisha. Ni uchaguzi wa kumpenda Mungu na watu wengine ili kwamba hatia, huzuni na pambano la ubinafsi liweze kuachwa nyuma. Tunaweza kusimama katika mwanga na furaha ya uhuru wa kweli. Je, utaufanya huo uchaguzi wa maisha hivi leo?
V. Juma lijalo: Kuishi kwa Kuongozwa na Roho Mtakatifu.

Subscribe to:
Posts (Atom)